Michuano ya kombe la dunia leo inaendelea tena kwa mechi tatu kupigwa katika viwanja tofauti nchini Urusi, Ufaransa leo inaumana na Peru katika mchezo wa kundi C uwanja wa Ekaterinburg Arena.
Ufaransa inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kutinga hatua ya 16 bora ya mtoano, Ufaransa iliishinda Australia mabao 2- 1 wakati Peru ilipoteza dhidi ya Denmark kwa bao 1-0.
Mchezo mwingine kundi C ni kati ya Denmark na Australia ambao unatarajia kuanza kabla ya mechi ya Ufaransa, mchezo wa mwisho utakaopigwa saa 3 usiku ni kati ya Argentina na Croatia utakaopigwa uwanja wa Nizhni Arena utakuwa ni wa kundi D