Yanga yatobolewa matatu na Azam Fc

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam Fc usiku huu imeilaza Yanga Sc mabao 3-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kufunga pazia.

Azam Fc walianza kuandikisha kalamu ya mabao kupitia kwa Yahya Zayd dakika ya 4 kipindi cha kwanza ambalo lilidumu hadi mapumziko, kipindi cha pili Yanga walirudi na kasi na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mateo Antony dakika ya 49 kabla ya dakika ya 51 Azam kuongeza bao la pili lililofungwa na Shaaban Iddi Chilunda na dakika 67 Salum Abubakar akaiandikia Azam bao la tatu.

Kwa matokeo hayo Azam imemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Simba ikifikisha pointi 58 huku Yanga ikiwa ya tatu na pointi zake 52

Azam imetoboa matundu matatu kwa Yanga leo