Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imeshindwa kuondoka na pointi tatu muhimu baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na masarange wa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Yanga ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kulisakama lango la Ruvu Shooting lakini washambuliaji wake hawakuwa makini na kujipatia magoli, Yanga waliandika bao la kuongoza kunako dakika ya 18 lililofungwa na Matheo Antony aliyepasiwa na Thabani Kamusoko, Goli hilo halikudumu kwani beki wa Yanga Abdallah Shaibu "Ninja" alounawa mpira na mwamuzi aliamuru ipigwe penalti iliyowekwa kimiani na Khamis Mcha "Vialii".
Yanga waliongez bao la pili katika dakika ya 36 lililofungwa na chipukizi Maka Edward aliyepasiwa na Pius Buswita, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao hayo, kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini Ruvu Shooting walikuja na kasi na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Issa Kanduru dakika ya 47