Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC leo inawakaribisha timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga inaweza kupata ushindi wake wa kwanza baada ya mechi tisa bila kupata ushindi ikiwa chini ya makocha wake wa muda, Mzambia Noel Mwandila na msaidizi wake Shadrack Nsajigwa.
Pia mabingwa hao wa zamani wanaipigania nafasi ya pili ambayo inakaliwa na Azam FC yenye pointi 55 wakati Yanga yenyewe iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 48 na bado ina mechi tatu mkononi hivyo inaweza kumaliza kwenye nafasi hiyo ya pili,hata hivyo Yanga inayotumia kikosi mchanganyiko na cha pili inaweza isipate mtelemko kwa vijana hao wa Mbao FC ambao nao wanataka kubaki Ligi Kuu na kuendeleza ubabe wao kwa Yanga.