Yanga kuipapasa Ruvu Shooting leo?

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa mechi moja kupigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwakutanisha mabingwa wa zamani Yanga Sc na Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani mchezo ambao unatajwa kuwa mkali na wa kusisimua.

Yanga ambao wameonja ushindi wa kwanza tangu alipoondoka kocha wake mkuu, Mzambia George Lwandamina inashuka dimbani jioni ya leo ikitaka kuendeleza wimbi lake la ushindi ili kuifukuzia Azam FC iliyo katika nafasi ya pili.

Lakini vijana wa Ruvu Shooting yenye msemaji wake mwenye maneno mengi, Masau Bwire hawatakubali kupapaswa na vijana hao wa Jangwanj kwani nao wanataka kujenga heshima na kuibuka na ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wake, kinachosubiriwa ni dakika 90

Yanga inaumana na Ruvu Shooting leo