Na Mwandishi Wetu. Kenya
Waandaaji wa michuano wa soka ya Sportpesa Super Cup 2018 wamepiga marufuku vilabu vitakavyowatumia wachezaji wapya na kutaka kila klabu itakayoshiriki michuano hiyo kutumia wachezaji wake walewale waliocheza ligi.
Michuano ya mwaka huu inatarajia kuanza Juni 3 kwa mchezo kati ya mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Simba Sc na Kariobangi Sharks ya Kenya na kufuatiwa na watani wao Yanga siku inayofuata Juni 4 ikicheza na Kakamega Homeboys pia ya Kenya.
Michuano hiyo ambapo bingwa hujipatia dola 30,000 na kupata tiketi ya kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton, itaendelea tena Juni 4 Singida United ikiumana na AFC Leopards na Gor Mahia itacheza na JKUya Zanzibar, tayari Simba na Yanga zimeshaanza kusajili wachezaji wapya na zikitaka kuwajaribu katika michuano hiyo hivyo sasa hawaturuhusiwa kuwatumia