ULIMWENGU ASAINI MIAKA MIWILI EL HILAL

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu ya Al Hilal ya Sudan baada ya kuachana na AFC Eskilistuna ya Sweden.

Ulimwengu aliachana na Eskilistuna baada ya kupata majeraha ya muda mrefu akitibiwa nchini Afrika Kusini, Al Hilal inayoshiriki Ligi Kuu ya Sudan ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi imeamua kumnasa straika huyo baada ya kuridhika naye.

Ulimwengu aliibukia TP Mazembe ya DRC ambapo aliitumikia vizuri sambamba na mwenzake Mbwana Samatta ambaye akauzwa Ubelgiji katika klabu ya Genk huku yeye akitua Eskilistuna ya Sweden ambayo nayo ikaachana nayo baada ya majeraha, hata hivyo dau alilonunuliwa Ulimwengu limebaki kuwa siri kwakuwa mchezaji huyo ni huru

Thomas Ulimwengu (Kulia) amejiunga na El Hilal ya Sudan