Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kikosi cha wachezaji 20 cha Yanga Sc kinatarajia kusafiri kuelekea Nakuru nchini Kenya jioni ya leo kwa ajili ya kushiriki michuano ya Sportpesa Super Cup.
Yanga imewaacha nyumbani mshambuliaji wake Mzambia Obrey Chirwa, mabeki Juma Abdul na Kelvin Yondani lakini katika kikosi chake kinachoanza safari muda huu wamo Mzimbabwe Thabani Kamusoko, Ibrahim Ajibu na Mkongoman, Papy Kabamba Tshishimbi.
Kikosi kamili kinachoelekea Kenya ni pamoja na makipa Youthe Rostand, Ramadhan Kabwili, mabeki Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Abdallah Shaibu, Pato Ngonyani, Viungo Baruani Akilimali, Pius Buswita, Ibrahim Ajibu, Maka Edward, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Makapu, Said Musa, Papy Tshishimbi, Yusuf Mhilu na Raphael Daudi, washambuliaji ni Yohana Nkomola, Matheo Antony na Amissi Tambwe, Yanga itashuka dimbani Jumatatu ijayo kucheza na Kakamega Homeboys katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru