Sportpesa yawajaza manoti Simba

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa Tanzania leo imewapatia shilingi Milioni 100 klabu ya Simba ya Dar es Salaam ikiwa kama shukrani yao kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2017/18.

Akizungumza leo katika ofisi za Sportpesa Osterbay Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Abas Tarimba amesema kampuni yao imewapa Simba kiasi hicho kama sehemu ya masharti waliyokubaliana katika mkataba ambapo walikubaliana kwamba timu kama ikichukua ubingwa wa Ligi Kuu wataipa kiasi hicho nje ya kile walichoandikiana.

Tarimba ameongeza kuwa Simba itaongezewa zaidi fedha kama itachukua na ubingwa wa Afrika, Sportpesa pia inaidhamini Yanga ambao ni mahasimu wakuu wa Simba, nahodha wa Simba John Bocco alikabidhi kikombe kwa wakurugenzi wa kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Uingereza ikopitia Kenya na kutua Tanzania

Simba wamejazwa manoti leo na Sportpesa