Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kwa vyovyote mahasimu wa soka la bongo Simba na Yanga wakakutana tena nchini Kenya katika michuano ya Sportpesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 3 mwaka huu kwa mabingwa wa soka nchini, Simba kuumana na Kariobangi Sharks ya Kenya katika uwanja wa Afraha.
Juni 4 washindi wa tatu wa Ligi Kuu Bara, Yanga Sc wataumana na Kakamega Homeboys pia ya Kenya na kama timu hizo zitashinda kwenye mechi zao hizo basi zitakutana katika nusu fainali na kufanya timu hizo zikutane kwa mara ya tatu ndani ya mwaka huu.
Tayari Simba imeshatangaza kuyapania mashindano hayo na itasafirisha kikosi chake cha kwanza kilichotwaa ubingwa wa Tanzania Bara na dhamira yao mwaka huu ni kushinda taji la michuano hiyo ili wapate tiketi ya kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton kama wadhamini wa michuano hiyo wanavyotaka, Yanga nao wameahidi kutoa ushindani katika michuano hiyo baada yakushindwa kwenye ligi yanyumbani