Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba Sc imeondoka asubuhi ya leo kuelekea nchini Kenya kushiriki michuano ya Sportpesa Super Cup lakini katika kikosi chake imeachana na nyota wake karibu wote waliofanikisha ubingwa wa Bara wakiwemo vinara wa mabao, Nahodha John Raphael Bocco na Mganda, Emmanuel Okwi.
Pia mabingwa hao imewaacha Waghana wake wote beki Asante Kwasi, kiungo James Kotei na mshambuliaji Nicolaus Gyan, beki Mganda Juuko Murushid na Mrundi, mshambuliaji Laudit Mavugo.
Waliosafiri leo ni makipa Aishi Manula, Said Mohamed, mabeki Ally Salim, Ally Shomari, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili, Mohamed Tshabalala, viungo Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, washambuliaji ni Rashid Juma, Moses Kitandu, pia imemjumuhisha mshambuliaji wake mpya kutoka Majimaji Songea, Marcel Kaheza lakini kama ameenda kuralii tu kwani kanuni za mashundano hayo haziruhusu wachezaji wapya