Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba kupitia katika mtandao wa Whatsaap, wanaojulikana kama Simba Whatsaap wamemzawadia mchezaji wa klabu hiyo Shomari Salum Kapombe kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kipindi kifupi alichoitumikia Simba.
Kapombe alikuwa majeruhi wa muda mrefu na alikosa kucheza mechi nyingi za mzunguko wa kwanza mpaka wa pili hadi kupelekea kushutumiwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Zakaria Hanspoppe, wanachama hao wanaounda group la Simba Whatsaap wamekoshwa na uchezaji wa Kapombe na wakaamua kumtunza shilingi 500, 000 za Kitanzania.
Wanachama hao wamemzawadia fedha hizo jana baada ya kumualika na kupiga naye picha, Kapombe alirejea mzunguko wa pili na sasa amekuwa katika kikosi cha kwanza cha Simha na kuchangia kuleta ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano