Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji ameenda kufanya ibada ndogo ya Hijja katika mji wa Makka na Madina kama sehemu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kufuatia kumaliza vema msimu kwa kuiwezesha timu yake ya Genk kupata tiketi ya kushiriki European League msimu ujao.
Katika mtandao wake, Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameonekana akiwa na rafiki yake ambaye naye ni mchezaji wa Genk, Omar Colley wakiwa katika msikiti wa Haram wakiadhimisha ibada ya Ihram ambapo waumini wa Kiislamu wanaouruhusiwa kufika hapo ni wale wasiofanya maovu.
Eneo hilo linaloaminika kuwa ni la Mwenyezi Mungu, Samatta alienda kushukuru hasa baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zulte Weregem katika uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Samatta anatazamiwa kuwasili nchini hivi karibuni akijiandaa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya rafiki yake Ali Kiba