SALAMBA ASAINI SIMBA MIAKA MITATU

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Klabu ya Simba imeanza kufanyia kazi mapendekezo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli aliyewataka kubadilika na leo wamemsainisha straika wa Lipuli ya Iringa, Adam Salamba kwa mkataba wa miaka mitatu.

Salamba ilikuwa atue Azam Fc hasa baada ya uongozi wa Lipuli kukataa maombi ya Yanga Sc ambao walituma maombi ya kumuhitaji nyota huyo ili akawasaidie kwa mkopo katika michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah "Try Again" amethibitisha usajili wa mshambuliaji huyo chipukizi alifikishwa mbele ya bilionea Mohamed Dewji 'MO:

Adam Salamba (Wa kwanza kushoto) amesaini mkataba wa miaka mitatu Simba Sc