PLUIJM AWAAGA SINGIDA UNITED, WACHEZAJI WAMWAGA MACHOZI

Na Mwandishi Wetu. Singida

Kocha mkuu wa timu ya Singida United ya mkoani Singida, Mholanzi Hans Van der Pluijm amewaaga wachezaji, viongozi na mashabiki wa timu hiyo akiwa safarini kujiunga na mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam FC ya Chamazi Dar es Salaam.

Kocha huyo wa zamani wa Yanga SC aliyewapa ubingwa wa Bara mara mbili mfululizo pamoja na kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup alitumia muda mfupi kuwaaga Singida United.

Pluijm tayari amefanikiwa kuiingiza fainali timu hiyo ya Azam Sports Federation Cup ambapo itaumana na Mtibwa Sugar itakayopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha, baadhi ya wachezaji wa Singida United wamekiri kuwa watamkumbuka kocha huyo kwani alifanikiwa kuisuka timu hiyo na kuifanya iwe miongoni mwa timu tishio msimu huu

Kocha Hans Van der Pluijm amewaaga rasmi Singida United