Pazia la Ligi Kuu Bara kufungwa leo

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18 linafungwa leo kwa mechi nane kupigwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini, ligi hiyo inafikia tamati ikiwa bingwa ameshapatikana ambaye ni Simba SC.

Vita pekee iliyosalia ni ya kumsaka mshindi wa pili ambayo inawaniwa vikali na timu za Azam Fc na Yanga Sc ambao leo wanaumana usiku katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Azam wana pointi 55 na Yanga ina pointi 52 hivyo nafasi iko wazi kwa Yanga endapo itashinda ila Azam inahitaji sare.

Pia vita ipo kwa timu mbili za Ndanda Fc ya Mtwara na Majimaji Songea ambapo moja leo itaungana na Njombe Mji kushuka daraja.

Ratiba kamili hii hapa

Yanga Sc vs Azam Fc Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 2;00 usiku.

Majimaji Fc vs Simba SC uwanja wa Majimaji Stadium mjini Songea.

Kagera Sugar vs Lipuli Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Tanzania Prisons vs Singida United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Ndanda Fc vs Stand United Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mtibwa Sugar vs Mbeya City Uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro.

Mbao Fc vs Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Njombe Mji vs Mwadui Fc Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe na hii itakuwa mechi ya mwisho ya Ligi Kuu kuchezwa mjini Njombe

Ligi Kuu Bara inamalizika leo kwa timu zote 16 kushuka uwanjani