Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam
Unaambiwa hakuna kitu kinachotawala hisia za mtu yeyote kama mapenzi, Mapenzi kila kiumbe kilichoumbwa na mwenyezi mungu anayo, basi kinara wa mabao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Emmamuel Okwi raia wa Uganda anayekipiga katika klabu ya Simba ya Dar es Salaam humwambii kitu kwa wanadamu watano ambao mwenyewe amikiri anawapenda.
Akizungumza hivi karibuni na kituo kimoja cha redio, Okwi mwenye mabao 20 na aliyeisaidia klabu yake ya Simba kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara amekiri kukoshwa na kiwango cha Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko anayekipiga Yanga.
Okwi amedai katika wanasoka wote wanaosakata soka hapa nchini anampenda mno Kamusoko na huwa anafurahi mno anapomuona nyota huyo akicheza, lakini pia Okwi amedai anakoshwa mno na mwanamuziki anayetamba sasa Dogo Aslay na kinachomvutia ni sauti yake.
Ila anayemzimia zaidi ni mkewe ambapo ameweka wazi kuwa anampenda mno mzazi mwenzake huyo, hata hivyo Okwi amesema pia anawapenda pia Ommy Dimpoz na Nandy huku pia akimkumbuka mwanasoka wa zamani wa Simba, Haruna Moshi "Boban"