Ni Real Madrid mabingwa tena Ulaya

Timu ya Real Madrid ya Hispania usiku wa jana imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuilaza Liverpool mabao 3-1 mchezo wa fainali iliyopigwa katika uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine.

Liverpool ilipata pigo mapema dakika ya 30 baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Mmisri, Mohamed Salah kutolewa nje kufuatia kuumia, dakika ya 51 Real Madrid walipata bao baada ya kipa wa Liverpool, Karius kupiga mpira uliomgonga Karim Benzema na kuujaza nyavuni.

Lakini Msenegar Sadio Mane akaikomboa Liverpool dakika ya 59 baada ya kufunga bao zuri, vijana wa Real Madrid walisherehekea taji lao la 13 kufuatia mtokea benchi Gareth Bale kufunga mabao mawili dakika ya 64 na 83

Real Madrid mabingwa tena Ulaya