NI REAL MADRID AU LIVERPOOL KUBEBA NDOO YA ULAYA LEO

Fainali ya kusisimua kabisa inatarajia kupigwa usiku wa leo huko mjini Kiev,Ukraine kati ya wababe wa Ulaya, Real Madrid ya Hispania na Liverpool ya England kuwania ubingwa wa Champions League.

Hiyo inatajwa kuwa fainali kali na ya kusisimua kutokana na ushindani wa timu zote na mashabiki wa timu hizo walibyopaniana, fainali itakuwa ya kusisimua zaidi hasa pale washambuliaji wawili hatari wanapokutana.

Mo Salah raia wa Misri aliyekatika kiwango bora kabisa ataiongoza Liverpool ambapo huenda akaisaidia timu yake kubeba taji la sita tangia walipoanza kulinyakua miaka kadhaa iliyopita, Cristiano Ronaldo raia wa Ureno ataiongoza Real Madrid kutwaa taji la 13 na mara tatu mfululizo

Real Madrid na Liverpool zinaumana leo