Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mshambuluaji wa Yanga Sc, Mzimbabwe Donald Ndombo Ngoma amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam Fc imefahamika leo.
Taarifa zilizothibitishwa na viongozi wa Azam Fc zinasema kuwa Ngoma amesaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Yanga Sc ambao wamekubaliana kuvunja mkataba uliosalia mwaka mmoja, Ngoma alijiunga na Yanga mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe lakini hawakuwa na maelewano mazuri na kusababisha kukaa nje kwa muda mrefu akisingizia majeraha.
Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema Ngoma hakuwa na majeraha makubwa isipokuwa hakuwa na maelewano na uongozi, hata hivyo Azam imekubali kugharamia matibabu ya mchezaji huyo atakayepelekwa nchini Afrika Kusini kutazamwa vizuri na ataitumikia timu hiyo msimu ujao na mashindano ya kombe la Kagame yanayotarajia kuanza hivi karibuni