Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Winga wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyepata pia kung' ara katika vilabu vya Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga, Azam na Simba za Dar es Salaam pamoja na Free State ya Aftika Kusini, Fanja ya Oman na Mbeya City ya Mbeya, Mrisho Khalfan Ngasa leo atakuwa na majukumu mazito ya kuinusuru timu yake ya sasa ya Ndanda FC ya mjini Mtwara itakaposhuka uwanjani kuwaalika Mwadui FC ya Shinyanga mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mchezo huo unataraji kuanza saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara macho yote yataelekezwa kwa mkali huyo aliyewahi pia kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya West Ham ya Uingereza huku pia akiwa na rekodi ya kucheza na Manchester United alipojiunga kwa muda na timu ya Seatle Sounders ya Marekani.
Mbali ya Ngasa, Ndanda pia inamtegemea mshambuliaji wake Omari Mponda ambaye atawasuuza wakazi wa Mtwara, hivi karibuni Mwadui iliifunga Yanga bao 1-0 hivyo leo itakuwa kazi nyepesi kwa Ndanda, Ndanda iko katika janga la kushuka daraja kwani hadi sasa inashikilia nafasi ya 15 ikiwa na pointi 23 na leo inamaliza michezo yake endapo ikifungwa itakuwa imeaga Ligi Kuu Bara 2017/18