NDAYIRAGIJE RASMI SINGIDA UNITED

Na Mwandishi Wetu. Singida

Klabu ya Singida United ya mkoani Singida leo imethibitisha kumalizana na kocha wa zamani wa Mbao FC, Mrundi, Etienne Ndayiragije kuwa kocha wake mkuu hasa baada ya Mholanzi Hans Van der Pluijm kujiunga na Azam FC ya Dar es Salaam.

Ndayiragije amesaini mkataba wa miaka miwili na atakuwa na jukumu kubwa kuhakikisha anaiweka matawi ya juu klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Pluijm ambaye ameiweka katika nafasi za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara na vilevile kuiwezesha kuingia fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup ambapo bingwa wake huliwakilisha taifa katika michuano ya kombe la Shirikisho.

Ikumbukwe Ndayiragije alikuwa akiinoa Mbao FC naye akisifika kwa kuifanya timu hiyo kuwa ya ushindani akiiongoza kuzitisha Simba na Yanga na kuingia fainali ya Azam Sports Federation Cup mwaka jana, kocha huyo aliachana na Mbao FC mapema mwaka huu na kumuachia msaidizi wake Fulgence Novatus kuiongoza hadi sasa

Etiene Ndayiragije akimwaga wino kujiunga na Singida United