Na Albert Babu. Mlandizi
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatazamiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja tu ambapo utachezwa katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa wenyeji Ruvu Shooting watakapoialika Mwadui Fc ya Shinganga.
Mchezo huo unatajwa kuwa wa ushindani wa aina yake kwakuwa Mwadui Fc iliapa kuendeleza ubabe kwa Ruvu Shooting hivyo hapo ndipo utamua wa mchezo wenyewe utakapoonekana, vijana wa Mwadui Fc chini ya kiungo mshambuliaji Hassan Kabunda, Awadh Juma, Awesu Awesu na wengineo wanataka kudhihirisha kuwa Mwadui Fc haitaki utani.
Lakini Ruvu Shooting ya Masau Bwire nayo iko vizuri na nyota wake Full Maganga, Abdulrahman Musa, Issa Kandulu, Damas Makwaya na wengine nao wanataka kulinda heshima yao na kulipiza kisasi
