Na Exipedito Mataluma. Njombe
Timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Turiani, mkoani Morogoro jioni ya leo imepeleka simanzi katika mji wa Njomhe baada ya kuichapa timu ya Njombe Mji bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kusababisha timu hiyo kurejea ilipotoka.
Kipigo hicho kimefanya Njomhe Mji kushuka daraja na sasa itashiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara msimu ujao, bao ambalo limepeleka simanzi na vilio limefungwa na kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga ambaye katika siku za karibuni amekuwa mwiba mkali kwa timu pinzani.
Mtibwa Sugar sasa wanafikisha pointi 40 wakiwa katika nafasi ile ile ya saba, Ligi hiyo inaendelea tena usiku huu ambapo Azam FC wanaikaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi, tayari Simba SC imetawazwa kuwa nabingwa wa msimu huu wa 2017/18