MSEMAJI WA YANGA NDANI YA KASHFA NZITO YA UPIGAJI PESA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Dissmas Ten ameingizwa kwenye kashfa nzito na kudaiwa ameihujumu klabu hiyo katika mradi mkubwa wa kalenda na majarida ya klabu hiyo.

Yanga ilijiingiza katika biashara ya kutengeneza kalenda na majarida ambapo msemaji huyo inasemekana alikuwa mhusika mkuu kwenye biashara hizo lakini hadi sasa fedha zilizopatikana hazijulikani zilipo na akiulizwa mtendaji huyo anasema hajui.

Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo, zinasema kuwa mpango huo umeratibiwa na uongozi wa Yanga kwa njia ya majaribio na wanakiri kweli baadhi ya makampuni yamejitokeza kutangaza biashara zao katika jarida lililotolewa na klabu hiyo.

Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema ni kweli fedha za majarida na kalenda hazionekani lakini walitoa kwa majaribio tu na hakuna mdhamini aliyelipia fedha za matangazo isipokuwa walifanya kama kujaribu, naye Dissmas Ten alipohojiwa kuhusu hilo amesema kama Mkwasa na hakuna upigaji wowote kama baadhi ya watu wakihoji

Dissmas Ten