Mkwasa awatoa wasiwasi Yanga, adai hata Simba nao ni choka mbaya

Na Albert Babu. Dar es Salaam

Katibu mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amewatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wa Yanga kuwa timu yao itafanya usajili wa kishindo lakini haitaruhusu mchezaji wake mwingine kuhamia timu nyingine mpaka pale yenyewe itakaporidhia ama kumuuza.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mkwasa amesema hata watani zao Simba nao wana njaa ila wanachofanya sasa ni propaganda tu, kuhusu kumkosa Adamu Salamba na kutua Simba,Mkwasa amedai Lipuli na Simba ni damu moja hivyo isingewezekana wao kumpata Salamba.

"Yanga tunashikiriki michezo ya kimataifa ingemsaidia Salamba kuonekana nje ya nchi, amekwenda kujimaliza Msimbazi", amesema Mkwasa, kuhusu tetesi za kuondoka nyota wao kuanzia Juma Abdul, Papy Kabamba Tshishimbi, AndrewVicent 'Dante' na Kelvin Yondan wanaodaiwa kujiunga na Simba pamoja na Azam, Mkwasa amedai hakuna mpango kama huo.

Mkwasa ambaye aliwahi kuichezea na kuinoa Yanga miaka iliyopita, amesema Yanga haitakubali kumwachia mchezaji yeyote na sasa wako mbioni kuwaongeza mikataba mipya nyota wake waliomaliza, kuhusu Tshishimbi amedai bado ana mkataba wa mwaka mmoja hivyo timu inayomuhitaji iweke mpunga mezani

Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema hata Simba ina njaa kali