Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Baada ya kufanikiwa kuipandisha Ligi Kuu, klabu ya KMC ya Kinondoni imepanga kuachana na kocha wake Fred Felix Minziro imefahamika.
Akizungumza jana, kiongozi wa timu hiyo Suzan Massawe amesema wamepanga kuachana na Minziro na tayari wameshaanza mazungumzo na makocha wengine ambao watafaa kuinoa timu hiyo, kiongozi huyo ambaye ni mwanamama amedai Minziro alipewa kibarua cha kuipandisha Ligi Kuu na ameweza hivyo sasa wakati wa kusaka kocha wa kushindana na Simba na Yanga umefika.
Aidha kigogo huyo ambaye pia ni mtumishi wa Halmashauri ya Kinondoni amedai hawana mpango wa kumchukua kocha wa zamani wa Mbao FC, Mrundi, Etienne Ndayiragije ambaye pia anatajwa kujiunga na Singida United, amedai kocha huyo hatoshi kukinoa kikosi chao kwa vile ameshindwa kuiongoza Mbao Fc na imenusurika kutelemka daraja msimu huu