MBEYA CITY SASA NAYO YAWA KAMPUNI, YAIPIKU SIMBA KWA MKWANJA

Na Exipedito Mataluma. Mbeya

Timu ya Mbeya City Council Footbal Club ya jijini Mbeya imeingia katika rada za Simba baada ya wamiliki wake kuiingiza katika mfumo wa kampuni na ikisajiliwa kwa msajili wa makampuni (Brela) na sasa inajulikana kwa jina la Mbeya City Football Club Public Limited Company.

Akizungumza jana, mtendaji mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema mpango wa kuifanya Mbeya City kuingia katika mfumo wa kuuza Hisa ulianza tangu  mwanzoni mwa mwaka huu na amedai kwa sasa ni kampuni.

Mbeya City inakuwa klabu ya pili kuwa kampuni baada ya Yanga SC iliyoingia katika mfumo wa kampuni mwaka 2001, lakini wanachama wake wakaenda mahakamani kupinga Yanga kampuni, Simba imeingia katika mfumo wa kampuni na wanachama wake wamebariki hivyo sasa inakuwa klabu ya kwanza nchini kuingia kwenye utaratibu huo ikifuatiwa na Mbeya City inayomilikiwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.

Simba kupitia kwa mwekezaji wake mfanyabuashara, Mohamed "Mo" Dewji ameweka mezani shilingi Bilioni 20 kutaka kununua Hisa asilimia 49 wakati Mbeya City wenyewe wameweka mezani shilingi Bilioni 100 kuendesha klabu yao kupitia kampuni

Mbeya City sasa ni kampuni