KUTINYU AMFUATA DONALD NGOMA AZAM FC

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kiungo Mzimbabwe Tafadwa Raphael Kutinyu amejiunga na klabu ya Azam Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Singida United ya mkoani Singida, huo unakuwa usajili wa pili wa Azam Fc ambayo tayari imemsajili Mzimbabwe mwingine kutoka Yanga, Donald Ngoma.

Usajili wa Kutinyu ni mapendekezo ya kocha mpya wa Azam Fc,Mholanzi Hans Van der Pluijm ambaye naye alikuwa akiinoa Singida United na analizia kibarua chake keshokutwa Jumamosi akiiongoza timu hiyo itakapoumana na Mtibwa Sugar katika fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup.

Azam Fc pia inatajwa kumwania mlinzi wa kulia wa Yanga, Juma Abdul Mnyamani ambapo taarifa za awali zinasema beki huyo amemaliza mkataba na huenda akasaini mkataba wa kuitumikia Azam msimu ujao

Tafadzwa Kutinyu anajiunga na Azam Fc