KIROHO SAFI MEXIME AENDA KUMRITHI NSAJIGWA YANGA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime amrkubali kuachia ngazi katika klabu yake hiyo na kwenda kuwa kocha msaidizi wa mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Bara, Yanga Sc akichukua nafasi ya Shadrack Nsajigwa anayetarajia kufutwa kazi.

Tayari Mexime ameshaaga Kagera Sugar ambao wako mbioni kumalizana na kocha wa Mwadui Fc ili akachukue nafasi yake, Mexime alikuwa akitakiwa na Yanga tangu msimu uliopita lakini ikashindikana na sasa mambo yametimia kutua kwa kocha huyo mwenye rekodi nzuri ya kuifunga Simba, hivi karibuni Kagera Sugar iliifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa kukabidhiwa kombe la ubingwa wa bara Simba mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.

Mexime aliwahi kuichezea timu ya Mtibwa Sugar na Taifa Stars akihudumu kama nahodha na baadaye akawa kocha wa timu hiyo kabla ya kuhamia Kagera Sugar na msimu uliopita alitangazwa kuwa kocha bora

Mecky Mexime anaenda Yanga