Mlinda wa mlango wa zamani wa mabingwa wa soka nchini, Simba SC, Daniel Agyei amechaguliwa kuwa kipa bora katika Ligi Kuu nchini Ethiopia akiwa anaichezea timu ya Jimma Ketema FC.
Agyei alisajiliwa na Simba sambamba na mwenzake James Kotei lakini akaachwa kwa mizengwe na kusajiliwa makipa wengine watatu ambao ni Aishi Manula, Said Mohamed na Emmanuel Mseja huku yeye akitimkia nchini Ethiopia ambapo msimu huu ameonekana bora na kutunukiwa tuzo