Kipa wa Liverpool atishiwa kifo

Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius raia wa Ujeruman ametishiwa maisha yake baada ya kusababisha klabu yake ya Liverpool kufungwa mabao 3-1 na Real Madrid Jumamosi iliyopita katika mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev,Ukraine.

Karius aliruhusu mabao mawili ya kirahisi mno moja akimzawadia Mfaransa, Karim Benzema na lingine akimpa mtokea benchi Gareth Bale, Karim Benzema alifunga bao la kwanza dakika ya 51 baada ya kipa huyo kuupiga mpira bila uangalifu na kumgonga Benzema na kuuweka nyavuni.

Kipa huyo aliyejiunga na timu hiyo mwaka 2016 akitokea Mainz, alifungwa goli la kirahisi na Gareth Bale dakika ya 83 akifumua shuti la mbali ambapo kipa huyo aliufuata bila mafanikio na kuingia nyavuni, polisi mjini Merseyside wameimarisha ulinzi kwa kipa huyo pamoja na familia yake kufuatia vitisho hivyo toka kwa mashabiki wa Liverpool kupitia mitandaoni

Kipa Loris Karius wa Liverpool ametishiwa kifo na mashabiki kwa kufungisha