KAHEZA ATOBOA SIRI KILICHOMPELEKA SIMBA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Majimaji ya Songea ambayo jana imetelemka daraja, Marcel Boniventure Kaheza ametoboa siri iliyopelekea kujiunga na mabingwa wa soka nchini Simba Sc.

Akizungumza na Mambo Uwanjani,Kaheza aliyeifungua Majimaji mabao 14 amedai ameamua kuachana na timu hiyo kwakuwa hajalipwa fedha zake za usajili huku akicheleweshewa mshahara wake, Kaheza ambaye tayari amesaini mkataba wa miaka miwili Simba Sc amedai viongozi wa Majimaji wamechangiakuishusha daraja.

Mchezaji bora huyo wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara amedai kushangazwa na uongo wa viongozi wa Majimaji ambao wamechangia timu hiyo kupotea, Kaheza amesema yeye bado alikuwa na mapenzi na timu hiyo lakini kwakuwa hakuna fedha ameamua kujiunga na Simba ambao wamemuahidi maisha bora

Marcel Kaheza