Na Asher Maliyaga
Mwanamuziki nguli wa miondoko ya kizazi kipya, maarufu bongofleva, Nasibu Abdul "Diamond Platinum" ni kama amemjibu hasimu wake kimuziki, King Ally Kiba baada naye jana kuzindua kinywaji chake cha Bilauri chenye picha yenye sura yake.
Hayo ni mapinduzi mengine kwa msanii huyo ambaye tayari anamiliki mradi wa kuuza Karanga zinazojulikana kwa jina la Diamond Karanga huku pia akianzisha kituo chake cha televisheni pamoja na redio, pia Diamond anamiliki studio yake mwenyewe inayojulikana Wasafi Record akiwa na utitiri wa wasanii ambao wako chini yake na wakiendelea kuachia ngoma kila kukicha.
Uzinduzi huo wa kinywaji cha Diamond unaenda sambamba na mwenzake Ali Kiba "King Kiba" kuanzisha kinywaji chake cha Mofaya ambacho kimekuwa kikikubalika, hivyo Diamond anaingia katika ushindani mwingine na Kiba badala ya muziki