AZAM YAJIPANGA KUMREJESHA VIALI

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam FC imejipanga kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Khamis Mcha "Viali" anayekipiga Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, mabosi wa timu hiyo kwa sasa wanahaha kutaka kumchomoa kwenye timu hiyo.

Mcha ameonyesha kiwango kikubwa akiwa na Ruvu Shooting akiisaidia timu hiyo kupata matokeo mazuri kiasi kwamba msemaji wa timu hiyo akianzisha msemo wake binafsi unaokua kwa kasi "Kupapasa" akizitambia timu pinzani.

Mcha aliachwa kimakosa sambamba na nyota wengine akina Mudathir Yahya aliyeenda Singida United, Gardiel Michael akaenda Yanga, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aishi Manula na John Bocco waliojiunga na Simba, uongozi wa Azam umeweka wazi mpango wake wa kutaka kumrejesha kiungo huyo mshambuliaji ambaye jana aliifungia bao timu yake dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Uhuru

Khamis Mcha "Viali" anarejea Azam