Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC jana usiku imeifunga Tanzania Prisons mabao 4-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ushindi huo unaifanya Azam Fc kuendelea kukalia nafasi ya pili ikifikisha pointi 55 lakini imesaliwa na mchezo mmoja pekee ambao wataucheza dhidi ya Yanga SC ambao wanasuasua.
Magoli ya Azam katika mchezo huo yamefungwa na Shaaban Iddi Chilunda (Hat trick) na kiungo Frank Domayo wakati lile la Prisons lilifungwa na Mohamed Rashid kwa mkwaju wa penalti, jana pia timu ya Mtibwa Sugar imeizamisha Njombe Mji mabao 2-0 mechi ikipigwa nyumbani Njombe katika uwanja wa Sabasaba na kuishusha rasmi daraja timu hiyo