Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mkali wa kusakata kandanda Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na mkali wa kuimba Bongofleva, Ali Kiba ambaye pia ni balozi wa Tembo Tanzania wanatarajiwa kukutana katika mchezo wa soka Juni 9 mwaka huu.
Akizungumza na vyombo vya habari, mratibu wa pambano hilo la soka, Daniel Cleverest amesema wakali hao wataunda vikosi viwili na kuchuana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupata fedha ambazo zitasaidia vifaa na miundombinu mashuleni.
Ali Kiba ataunda kikosi chake cha wanasoka anaowafahamu yeye wakati Mbwana Samatta naye ataunda kikosi chake anachokifahamu na kutengeneza timu mbili zitazochuana siku hiyo, wawili hao ni marafiki na wamekubaliana kufanya hivyo likiwa ni jambo zuri kuigwa