ALBUM YA NGWEA YAJA

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Kundi la muziki wa kizazi kipya la Chemba Squad lenye maskani yake jijini Dodoma linatarajia kuachia album ya aliyekuwa nsanii wao marehemu Albert Mangwea 'Ngwea' itakayojumlisha baadhi ya nyimbo zake mpya na za zamani inatoka hivi karibuni.

Akizungumza jana wakati wa kuandhimisha kumbukumbu ya miaka mitano ya kifo chake, M To the P amesema ujio wa album ya Ngwea ndio mipango yao kwa sasa na amewataka wapenzi na mashabiki wa msanii huyo kujiandaa kupokea album hiyo.

M To the P ambaye alikuwa sambamba na Ngwea nchini Afrika Kusini kabla ya kufikwa na mauti huku naye akiwa hoi hospitalini, amedai wameamua kuitoa album ya Ngwea ili kurejesha enzi za kutamba kwa kundi lao na msanii huyo, aidha msanii huyo amewataka wasanii wanaotumia sauti ya Ngwea kuacha kufanya hivyo kwani sheria ya Hakimiliki itachukua mkondo wake

Marehemu Albert Mangwea