Na Mwandishi Wetu. Mtwara
Kikosi cha timu ya ndanda FC "Wana Kuchele" jioni ya leo kimeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Ushindi huo umeifanya Ndanda kusalia Ligi Kuu Bara na kusababisha timu ya Njombe Mji ya Njombe kutelemka daraja, Ndanda imefikisha pointi 26 na sasa inashikilia nafasi ya 14 ikiiacha nyuma Majimaji yenye pointi 24 atija nafasi ya 15 na Njombe yenye pointi 22 nafasi ya mwisho.
Magoli yaliyoibakisha Ligi Kuu Ndanda yamefungwa na Jacob Massawe kunako dakika ya 3, Mrisho Ngasa dakika ya 5 na Tibar John dakika ya 40, Ligi hiyo itaendelea tena Ijumaa ijayo kwa Yanga Sc kuikaribisha Ruvu Shooting uwanja wa Taifa Dar es Salaam