MTIBWA SUGAR HAWAKAMATIKI, WAILIPUA STAND UNITED NA KUTINGA FAINALI

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Timu ya Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu mkoani Morogoro jioni ya leo imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup baada ya kuilaza Stand United mabao 2-0 mchezo wa nusu fainali  wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Mchezo ulikuwa mkali kwa timu zote kushambuliana lakini Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuberi Katwila ilionekana kuutawala mchezo huo kipindi cha kwanza na kufanikiwa kufunga mabao yote mawili kupitia kwa kiungo mshambuliaji wake Hassan Dilunga kwenye dakika za 30 na 38.

Kipindi cha pili Stand United waliweza kulinda lango lao na kufanya mashambulizi mengi kwa Mtibwa lakini hawakuweza kupenya ukuta, Mtibwa sasa imetinga fainali ikisubiri mshindi kati ya Singida United na JKT Tanzania utakaopigwa Jumapili, bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Mtibwa Sugar imeingia fainali ya FA Cup ikiifunga Stand United 2-0 leo