Busungu, Mwaisabula waiongezea mzuka Lipuli kuia Simba

Na Ikram Khamees. Iringa

Kuwepo kwa kocha mzoefu na mchambuzi mahiri wa soka nchini, Kenny Mwaisabula "Mzazi" kwenye kikosi cha Lipuli Fc ya Iringa na uwepo wa mshambuliaji Malimi Busungu kunaiongezea mzuka Lipuli kuilaza Simba leo.

Wawili hao wapo Iringa na kikosi cha Lipuli huku kila mmoja akiwa na jukumu lake, Mwaisabula yeye amewahi kuzinoa Bandari ya Mtwara, Cargo ya Dar es Salaam, Yanga Sc na JKT Tanzania zamani JKT Ruvu na anawajua vilivyo wachezaji wa Kitanzania.

Wakati Busungu yeye amekuwa na rekodi nzuri ya kuitungua Simba kila timu anayojiunga nayo, amewahi kuiliza Simba alipokuwa Polisi Moro (Sasa Polisi Tanzania) pia amefanya hivyo akiwa na JKT Mgambo, Yanga Sc na sasa yupo Lipuli na leo wanakutana na Simba ngoja tuone kama atawalaza mapema Wekundu hao wa Msimbazi wanaokamata usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 58 zikiwa ni nyingi mno kuliko anayefuatia Yanga mwenye pointi 47

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI