MANYIKA JR AREJEA KUITIBULIA YANGA

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Kipa namba moja wa Singida United, Peter Manyika Jr hatimaye amerejea uwanjani baada ya kukosekana kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake.

Taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Singida United zinasema kuwa kipa huyo huenda sasa akakaa langoni kuivaa Yanga katika mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup hapo Aprili 1 hatua ya Robo fainali itakayopigwa uwanja wa Namfua mjini Singida.

Manyika Jr amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho na kurejea kwake kunaibua hofu kwa mabingwa wa soka nchini Yanga Sc ambao wanaijua vema shughuri ya mlinda mlango huyo ambaye ni mtoto wa kipa wao wa zamani, Manyika Peter Manyika

Peter Manyika Jr amerejea tena langoni