Na David Pasko. Dar es Salaam
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete na waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, wamewaongoza mamia ya wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga kumzika aliyekuwa mchezaji wao na timu ya taifa, Taifa Stars, Athuman Juma Chama 'Jogoo'.
Chama amezikwa leo Dar es Salaam baada ya kufariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikolazwa kwa muda mrefu akiugua Kiharusi.
Kikwete ambaye pia amewahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga mwaka 1976 na kufanikiwa kumsajili mchezaji Shabani Katwila, aliwaongoza Wanayanga katika mazishi hayo ambayo pia yaliudhuriwa na aliyekuwa mpenzi na mwanachama wa klabu hiyo Mwigulu Nchemba ambaye kwa sasa amejiunga na timu ya nyumbani kwao Singida United.
Marehemu Chama alijiunga na Yanga mwaka 1981 akitokea Pamba Fc ya Mwanza, na alipachikwa jina la Jogoo baada ya kumdhibiti mshambuliaji wa Simba enzi hizo Zamoyoni Mogella.
Mogella alikuwa akikabwa hata akienda kunywa maji ambapo beki huyo alikuwa akimfuata kwa nyuma, ambapo mashabiki wakampachika jina la Jogoo wakimfananisha na kuku jogoo
