Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Staa Wetu

Joseph Marius Omog. Shujaa aliyefia vitani.

Na Prince Hoza

SIKUWEZA kuamini pale niliposikia kocha mkuu wa Simba SC, Mcameroon Joseph Marius Omog amefutwa kazi kuinoa timu hiyo, sikuamini kabisa taarifa hiyo ya kufutwa kazi, taarifa ilianzia kusambaa kwenye mitandao ya kijamji mchana.

Mitandao ya kijamii siku hizi haiaminiki sana kwakuwa kuna watu wamekuwa wakisambaza uongo, na ndio maana watu wenye heshima zao hawataki kuamini haraka taarifa zinazosambazwa mitandaoni, ilikuwa haraka kuamini Abdallah Kibaden "King" kuwa amefariki dunia.

Kuna watu walieneza uzushi huo kuwa Kibaden amefariki wakati si kweli, ndivyo nilivyoshindwa kuamini kama Omog amefutwa kazi Simba.

Lakini nilikuja kuamini pale niliposikia Afisa Habari, Haji Manara akithibitisha, Omog alitimuliwa kazini baada ya Simba kutolewa katika michuano ya Azam Sports Federation Cup, (ASFC), maarufu kombe la FA.

Wekundu hao wa Msimbazi walifungwa na timu ya daraja la pili ya Green Warriors kwa mabao 4-3 yaliyotokana na mikwaju ya penalti kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, kwa maana hiyo Simba imevuliwa ubingwa wa mashindano hayo.

Ikumbukwe Omog aliiongoza Simba msimu uliopita kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya FA baada ya kuilaza Mbao FC mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Simba imepata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrija mwakani kupitia michuano hiyo ya Azam Sports Federation Cup, (ASFC) ikiwa chini ya Mcameroon, wamepita makocha zaidi ya sita Simba ikiishia kuitwa wa mchangani pasipo kupata uwakilishi wa mashindano ya kimataifa lakini Mcameroon huyo akaiondolea Simba aibu hiyo.

Baada ya Simba kufungwa na Green Warriors, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Sundau Manara alianza kuandika katija ukurasa wake wa Instragram kuwa ameumia sana Simba kutolewa mapema, Manara alifunguka kuwa tangia alipoanza kufanya kazi Simba hajawahi kuumia kama alivyoumia kwa kutolewa na Green Warriors kwa mikwaju ya penalti.

Ina maana Manara hakuumia wakati Simba ikigeuzwa mteja kwa kufungwa mara mbili mfululizo dhidi ya mahasimu wao Yanga SC, Simba ilifungwa mabao 2-0 kila mchezo 2015/16, ina maana Manara hakuumia Simba ilipoukosa ubingwa wa Bara msimu uliopita hasa baada ya kulingana pointi na Yanga.

Nina hakika penalti hazina mjuzi, timu yoyote inapofikia hatua ya kupigiana penalti lolote linaweza kutokea, lakini Manara akawa wa kwanza kuumia, mtu mwingine aliyeumia ni Mohamed Dewji "Mo" ambaye naye alipost katika ukurasa wake wa Twitter.

Mo aliandika maneno yaliyomtaka kocha mkuu Joseph Omog kujiuzuru, kitu ambacho kilipelekea Mcameroon huyo kubwaga manyanga, kocha huyo mbali na kuonekana tatizo kwenye klabu ya Simba kiasi kwamba alianza kuandamwa na mashabiki.

Mashabiki wengi wa Simba walitaka ajiuzuru huku wengibe waliutaka uongozi wa Simba unfute kazi, sababu kubwa ambayo ilikuwa ikitajwa eti kwanini anawaweka benchi Mohamed Ibrahim "Mo" na Jonas Mkude, lakini wamesahau umahiri wake, wanasahau mbinu na mikakati yake ya ufundishaji.

Omog ni kocha mwenye mbinu na mikakati ya hali ya juu na ndio maana amekuwa na mafanikio kila anapoiongoza timu, kocha huyo amekuwa na mifumo tofauti pindi anapoiongoza timu kulingana na wachezaji alionao, na hiyo imepelekea Simba mpaka sasa kucheza mechi 11 za VPL bila kufungwa.

Omog alipata kazi ya kuinoa AC Leopards ya Congo Brazaville, timu ambayo aliikuta inasota kwa misimu kadhaa bila kupata kikombe cha Ligi Kuu wala FA, Lakini Mcameroon huyo alipoanza kazi aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa nchi.

Timu hiyo ilipotwaa ubingwa wa nchi ikapata tiketi ya kushiriki Ligi ya mabingwa barani Afrika, Omog aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Afrika, ndipo matajiribwq Azam walipoamua kuingia naye kandarasi ya miaka miwili, Azam FC walikuwa na hamu ya kutwaa ubingwa wa Bara.

Akiiongoza Azam FC katika msimu wake wa kwanza 2013/14 akaiwezesha kutwaa ubingwa wa bara bila kupoteza mchezo, Na pia ilipata tiketi ya kushiriki Ligi ya mabingwa barani Afrika, kwa bahati mbaya timu hiyo haikufanya vizuri.

Omog amezaliwa Novemba 30, 1971 Younde, Cameroon, kocha huyo aliajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akichukua mikoba ya Muingereza, Dylan Kerr, Omog akaanza kazi Simba SC na kukaribia kuipa ubingwa wa Bara isipokuwa ilitofautiana na Yanga magoli ya kufunga huku zote zikiwa sawa kwa pointi.

Lakini akafanikiwa kuipa ubingwa wa FA na kuingia michuano ya kimataufa mwakani, na pia Omog ameiweka Simba SC kileleni ikiwa na pointi 23 sawa na Azam ila ina mabao mengi ya kufunga na imecheza mechi 11, Omog ni shujaa aliyefia vitani, Simba kwa sasa inanolewa na kocha msaidizi  Masoud Djuma raia wa Burundi akisaidiana na kocha wa makipa Muharammi Mohamed "Shilton".

Joseph Omog amefutwa kazi Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC