CHALENJI YAIPOROMOSHA TANZANIA VIWANGO FIFA

Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Baada ya kuvurunda katika michuano ya kombe la Chalenji, Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano zaidi kwa mwezi Desemba katika viwango vya ubora wa kutandaza kandanda ulimwenguni vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la mpira wa miguu duniani, (FIFA).

Katika viwango vilivyotolewa na Shirikisho hilo na kutangazwa leo, Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 142 hadi 147 huku Uganda ikiendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika mashariki na vilevile kukamata nafasi ya 75 kwa Afrika.

Kuporomoka kwa Tanzania kumechangiwa zaidi na matokeo mabovu iliyoyapata katika michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, maarufu Chalenji yaliyomalizika juma lililopita na Kenya kutwaa ubingwa kwa kuifunga Zanzibar kwa mikwaju ya penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120

Tanzania imeporomoka tena FIFA

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI