Mchezo wa fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika umefanyika jana usiku kwenye mchezo ukifanyika Morocco, Wydad Casablanca kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 Dhidi ya Al Ahly ya Misri
Goli la Wydad Casablanca limefungwa na Walid El Karty mnamo dakika ya 69.Katika Mchezo wa awali uliochezwa nchini Misri timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli 1-1 hivyo matokeo kwa ujumla yanakuwa Wydad Casablanca 2-1, Al Ahaly
Wydad Casablanca unakuwa ubingwa wao wa pili kutwaa taji la Klabu Barani Afrika mara ya Mwisho walitwaa taji hilo mwaka 1992 walipoifunga All Hilal ya Sudan
