Kagera Sugar waona mwezi, Mtibwa yang' ang' aniwa nyumbani

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara leo imeendelea kwa mechi tano ambapo Kagera Sugar kwa mara ya kwanza imeona mwezi baada ya kuilaza Ndanda FC mabao 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Kaitaba mjini Bukoba na kufikisha pointi sita.

Ndanda walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa na mshambuliaji wake Omary Mponda lakini Venance Ludovic aliisawazishia Kagera bao kabla ya Christopher Edward kuifungia bao la ushindi.

Matokeo mengine ni kama ifuatavyo: Mtibwa Sugar 0 Singida United 0, Lipuli FC 2 Mbao FC 1, Majimaji FC 1 Mwadui FC 1,  Njombe Mji 0 Stand United 0, Ligi hiyo itaendelea tena  kesho kwa mchezo mmoja kati ya Prisons na  Ruvu Shooting

Kagera Sugar wakishamgilia ushindi wao wa kwanza