Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania na timu ya Diffaa El Jadida Ya nchini Morrocow Saimon Msuva Ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi August katika timu yake, Msuva amekuwa katika kiwango kizuri tangia alipojiunga na timu hiyo akitokea Yanga SC ya Tanzania ambayo aliipa ubingwa wa bara mara tatu mfululizo huku akimaliza kama mfungaji bora.
Hiyo ni hatua nzuri kwa Msuva ambaye ndiye mara yake ya kwanza anajiunga na klabu hiyo akicheza mechi sita za kirafiki na moja ya ligi, mafanikio ya Msuva yameonekana hivi karibuni pale alipoweza kuifungia Tanzania mabao mawili katika ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Botswana mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
