Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Makala ya Kispoti

TUNAPANDAJE VIWANGO KWA KUCHEZA NA MALAWI!

Na Prince Hoza

KWANINI Watanzania hasa wapenda soka wanaendelea kumkumbuka Rais Leodegar Chila Tenga ni kwa sababu aliiwezesha timu ya taifa, Taifa Stars kucheza na vigogo wa soka barani Afrika, wakumkumbuka mwingine ni aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mbrazil Marcio Maximo.

Kingine labda niseme kocha wa sasa wa Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga ni muoga wa mechi, labda hapo naweza kueleweka kidogo maana tumechoka kusikia timu yetu ya taifa kila inapokuja kalenda ya FIFA tunacheza na Malawi au Burundi.

Nasema tumechoka, mwezi ujao wa Oktoba 7 mwaka huu, Taifa Stars itacheza na Malawi mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwa maana hiyo Stara inaingia kambini Oktoba 1 Jumapili ijayo na Oktoba 7 watacheza na The Flame, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itasimama kupisha mchezo huo, tayari kocha Mayanga ameita wachezaji 22 kwa ajili ya mchezo huo.

Mayanga ameshindwa kuwashawishi TFF kupata mechi kubwa za kirafiki ambazo nadhani zingeweza kuibadili timu hiyo, kwa sasa Tanzania inakamata nafasi 125 katika viwango vya FIFA vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho hilo la mpira wa miguu duniani.

ENZI ZA LEODEGAR TENGA

Wakati ule Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) likiongozwa na Rais wake Leodegar Tenga ambaye amewahi pia kuichezea timu ya taifa akicheza kama beki wa kati, Tenga hakuwa mwoga alitafuta mataifa yenye uwezo mkubwa kisoka kupita Tanzania ili kucheza nazo mechi za kirafiki.

Nadhani Tenga alikuwa akisikiliza ushauri mzuri kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa, Marcio Maximo, Tanzania ilipata nafasi ya kuzialika timu tulizokuwa tukizisikia redioni ama kuziona katika runinga, mataifa kama Ghana, Ivory Coast, Cameroon na nyinginezo ziliweza kukanyaga ardhi ya Tanzania kucheza na Stars.

Na kwa bahati nyingine mataifa hayo yaliweza kuja na mastaa wake wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya, tukawashuhudia akina Samuel Eto' o "Fills", Didier Drogba wakija Tanzania, mastaa hao walikuwa wakicheza Ulaya na waliogopeka kwelikweli.

Eto' o alikuwa akiichezea FC Barcelona wakati Drogba alikuwa Chelsea, jina la Tanzania lilizidi kujulikana nje ya mipaka yetu, na pia tulipata uzoefu wa kutosha na ndio maana tuliweza kuwafunga Morocco, alipoondoka Tenga akaja Jamal Malinzi ambaye alianza kufanya kazi na benchi lingine la ufundi.

Malinzi naye alifuata nyayo za mtangulizi wake lakini akaja kuua misingi hiyo na kujikuta anakaribisha timu jirani za Burundi na Malawi katika mechi za kirafiki za Fifa, kwa bahati mbaya nchi hizi viwango vyao viko chini tofauti na Cameroon, Zambia, Ivory Coast, Senegar na Ghana au Mali.

Timu yetu imekuwa ikibadilishana kucheza na Malawi au Burundi kila mechi za Fifa zinapopangwa, na sasa TFF inaongozwa na Wallace Karia na Oktoba 7 itacheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Malawi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Si kwamba naibeza Malawi au Burundi, isipokuwa naona kama tunapoteza bure muda wetu,tumechoka kuwatazama Malawi kila mara, binadamu anapenda mabadiliko, na ndio maana asubuhi tunakunywa chai au kahawa, mchana tunakula ugali, ubwabwa au makande na usiku pia tunakula chakula kingine.

Wapo wanaofululiza kula ugali wakati wote au ubwabwa wakati wote lakini utakuta wanabadili mboga, Malawi tumemchoka tungependa kuona timu yetu ya taifa ikiialika Ghana, Senegar, Mali, Angola au Nigeria, sidhani kama mataifa hayo yanaweza kutugomea kucheza nazo.

Kwa sasa Tanzania tayari imeshajitangaza hivyo haitakuwa na ugumu kupata mechi kubwa kubwa, kwangu mimi namuona kocha Salum Mayanga anaogopa kivuli chake,Mayanga anaogopa kucheza na mataifa yanayojua mpira akiogopwa kufungwa.

Mpaka sasa kocha huyo amejiwekea rekodi nzuri lakini rekofi yenyewe ukiiangalia utachoka mwenyewe, mechi nyingi amecheza na Malawi, kwakweli umefika wakati sasa kocha na Rais wa TFF kubadilika, tuleteeni mataifa yenye nguvu kidogo na siyo kutuletea timu tulizozoeana nazo kila mara tunajichukulia alama kutoka mikononi mwao.

Mchezo huo wa Stars na Malawi Oktoba 7 unatuharibia utamu wa Ligi Kuu Bara ambayo tayari imeanza kuwa tamu, ligi imekuwa tamu kwa sababu kuna ushindani mkubwa katika kufukuzia usukani.

Mtibwa Sugar na Azam FC zinakabana koo katika msimamo wa ligi zote zikiwa na pointi 10 tofauti yao kwenye mabao ya kufunga na kufungwa, utamu huo unanogeshwa na Singida United na Tanzania Prisons ambazo zimeonyesha utamu wa ligi hiyo, safari hii Simba na Yanga zimeachwa nyuma kabisa, lakini hiyo siyo mada yangu ya leo, wacha nikapumzike niendelee na majukumu mengine nasema Kwaherini

Kikosi cha Taifa Stars Oktoba 7 mwaka huu kitaumana na Malawi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC