Kiungo Yanga, aachia video ya "Wanatupa watoto"

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Kiungo wa zamani wa Yanga B, Abdul Zen "Okocha" amekamilisha video ya wimbo wake wa miondoko ya Hip hop "Wanatupa watoto" ambayo tayari ameisambaza katika mitandao ya kijamii na imepokelewa vema na mashabiki wake.

Abdul  Zeni amewahi kuichezea Yanga B wakati ule ikinolewa na marehemu Tambwe Leya na ilikuwa kidogo apandishwe kwenye kikosi cha wakubwa isipokuwa aliumia, na sasa amegeukia muziki wa kizazi kipya na tayari ana albamu.

Tayari msanii huyo ameshatambulisha video yake nyingine ya wimbo wa mapenzi lakini video ya wimbo huu unaohusu utupaji wa watoto, Abdul Zeni ameonyesha masikitiko yake kwa watu wenye tabia ya kutupa watoto hasa vichanga

Abdul Zeni, mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anajisghurisha na muziki